Jeremiah 5:9-14


9 aJe, nisiwaadhibu kwa ajili ya hili?”
asema Bwana.
“Je, nisijilipizie kisasi
juu ya taifa kama hili?


10 b“Piteni katika mashamba yake ya mizabibu na kuyaharibu,
lakini msiangamize kabisa.
Pogoeni matawi yake,
kwa kuwa watu hawa sio wa Bwana.

11 cNyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda
wamekuwa si waaminifu kwangu kamwe,”
asema Bwana.


12 dWamedanganya kuhusu Bwana.
Wamesema, “Yeye hatafanya jambo lolote!
Hakuna dhara litakalotupata;
kamwe hatutaona upanga wala njaa.

13 eManabii ni upepo tu, wala neno halimo ndani yao,
kwa hiyo hayo wayasemayo na yatendeke kwao.”

14 fKwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote: “Kwa sababu watu hawa wamesema maneno haya,
nitayafanya maneno yangu vinywani mwenu kuwa moto,
na watu hawa wawe kuni
zinazoliwa na huo moto.
Copyright information for SwhKC